wanjikusblog - Wanjiku's two cents.
Wanjiku's two cents.

148 posts

Sauti, Usemi, Na Mashairi Yake Abdalla.

Sauti, usemi, na mashairi yake Abdalla.

Swahili poet and longtime political activist Abdilatif Abdalla recites his only English language poem "Peace, Love, and Unity for whom?"

Profesa Abdilatif Abdalla anaonekana hapa akilikariri shairi lake la "Peace love and unity for whom?" Shairi ambalo aliliandika kana kwamba kukejeli falsafa yake Daniel Moi ya Amani, Upendo, na Umoja. Msomaji, utakumbuka kwamba Daniel Moi kwa wakati mmoja amemtumia vijumbe profesa akiwa uhamishoni pale Tanganyika, eti kwa minajili ya kumshawishi na kumhonga profesa aachane na harakati zake hizo za kupigania haki.

Na zaidi ya kuyatunga mashairi yenye mafumbo na mafunzo mbali mbali, profesa Abdalla amewahi kuwa mhadhiri katika idara ya Kiswahili pale chuo kikuu cha Leipzig na pia London. Katika uandishi wake Abdalla amezitumia lahaja mbali mbali zikiwemo Kimvita, Kingwana cha Congo, Kingazija cha Comoros, Kimrima cha Dar, na kadhalika. Si ajabu Profesa Abdalla amechangia kwa ukubwa ubunifu na uhifadhi wa lugha ya Kiswahili.

Ingawa Abdalla si mwandishi wa mara kwa mara, mashairi yake yamesomwa na wengi. Na imekuwa dhahiri kutoka ujana wake, kwamba utunzi ni kipawa cha kiasili alichotunukiwa Abdalla. Kuambatana na hiyo hamu na ghamu ya utunzi wa mashairi, profesa ameiandika antholojia yake ya kwanza Sauti yadhiki (1973), akiwa kijana chipukizi wa miaka ishirini na miwili. Kwa wakati huo, Jomo Kenyatta alikuwa amemtia Abdalla korokoroni kwa shitaka la uhaini eti kwa sababu Abdalla alichapisha kijitabu chake cha “Kenya Twendapi?”

Tags

More Posts from Wanjikusblog

1 year ago

As a matter of fact BBC, you'd be surprised to learn that Kilifi isn't the only area of this country where tiki torch wielding crazies accuse the elderly of being witches for the sole purpose of murdering old people in order to steal their land.

#justice

1 year ago

Probably one of the most iconic moments in recent history. The Unknown Protester stands unmoved against a phalanx of Chinese tanks (Tiananmen Square, June 5 1989).

#world politics

#global politics

wanjikusblog - Wanjiku's two cents.
1 year ago

Story za Jaba.

.... it took my entire ear off. The whole ear. But I went to the doctor, and he said, and this is true, he said, you heal faster than anyone I've ever seen. Nobody is healthier than you. And the next day, my ear was growing back, and the doctor said, nobody regrows ears like that, and it's a really remarkable thing, regrowing an ear like that, most people can't do it. And I know that, because it's not me saying this, it's the doctor, it's everybody saying, just, you're the best at regrowing ears.

#tall tales

#satire

1 year ago

Arts and crafts.

Fundi huyu mwenye ujuzi wa hali ya juu, ametengeneza kikapu ambacho kinaweza kugeuzwa kuwa kitu chochote, iwe meza, pambo la ukuta, hadi kikapu cha kuhifadhia vyakula kama vile chapati, nk.

#arts & crafts